Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu Fabrice Ngoma, fundi haswa aliyetumwa kazi Msimbazi

Fabrice Ngoma Ses.jpeg Fabrice Ngoma

Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leo kKlabu ya Simba imemtambulisha Fabrice Luamba Ngoma kuwa mchezaji mpya kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili utakaomwezesha kukaa Msimbazi hadi mwaka 2025. Ngoma ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DR Congo) na kwa sasa ana umri wa miaka 29, akiwa amezaliwa Januari 22, 1994.

Maisha yake ya soka la ushindani yalianzia kwenye timu ya MK Etancheite ya DR Congo mwaka 2015 na baada ya hapo alisajiliwa na Ifeanyi Ubah ya Nigeria mwaka 2017 ambapo alicheza kwa miezi sita kabla ya kurudi DR Congo kujiunga na AS Vita Julai 2017.

Akiwa AS Vita ambapo kulimtambulisha zaidi kwenye soka la kiushindani barani Afrika, mwaka 2019 aliuzwa kwa miamba ya Morocco, Raja Casablanca kwa ada ya uhamisho ya Dola 268,000.

Akiwa Raja aliiwezesha kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Morocco na Kombe la Shirikisho Afrika kabla ya mkataba wake kumalizika na kujiunga na Al Fahaheel ya Kuwait Agosti, 2022 na ilipofika Januari 2023 alikamilisha uhamisho wa kutua Al Hilal ambapo amedumu kwa miezi sita kabla ya kutua Simba ambapo amesaini mkataba wa miaka miwili.

Kwenye upande wa michuano ya kimataifa, staa huyu amecheza mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika na kufunga mabao matatu na vilevile kwenye Shirikisho amecheza mechi 23 akifunga mabao sita na asisti nne.

Pia amewahi kucheza mechi 17 akiwa timu ya taifa ya DR Congo akianzia mwaka 2018 na mara ya mwisho kuitwa ilikuwa Septemba, 27, 2022 ambapo alikaa benchi kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Sierra Leone.

Mchezaji huyu ana uwezo wa kucheza sehemu nyingi uwanjani za kiungo na mara kadhaa ameonekana akicheza kama beki wa kati, ingawa muda mwingi hucheza kiungo wa kati. Vilevile anaweza kucheza kama kiungo mshambuliaji, kiungo mkabaji na winga wa kushoto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: