Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mechi ya Simba vs Singida yabadilishiwa muda

Simba Vs Singida.jpeg Mechi ya Simba vs Singida yabadilishiwa muda

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Ligi Kuu Bara imebadilisha muda wa mchezo wa Simba na Singida Fountain Gate ambao ulipangwa kuchezwa saa 10 jioni na sasa utachezwa saa 1:30 usiku, Azam Complex Chamazi.

Akizungumza ofisa habari wa bodi hiyo Karim Boimanda, amesema sababu ya kubadilishwa muda wa mchezo zimetokana na mabadiliko ya uwanja.

“Mchezo huo awali ulipangwa kuchezwa katika Uwanja wa Jamhuri Morogoro, uwanja ambao hauna taa za kuruhusu kucheza usiku hivyo kwakuwa mchezo utachezwa Azam Complex na kuna miundombinu ya taa hakuna ulazima wa kucheza mechi mchana au jioni”

Hata hivyo, Boimanda ameongeza kuwa endapo itafika wakati viwanja vyote vilivyokidhi vigezo vya kuchezewa mechi za Ligi Kuu kuwa na taa, hakuna budi kucheza mechi hizo mchana au jioni, zitachezwa usiku wakati ambao mashabiki wameshatoka kwenye majukumu mengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: