Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchome Mapovu: Simba wanaamini ushirikina

Simba Ushirikina.jpeg Mchome Mapovu: Simba wanaamini ushirikina

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki kindakindaki wa Simba SC, Mchome Mapovu amesema kuwa klabu hiyo wana imani za kishirikina sana jambo ambalo linaifanya timu hiyo kukosa matokeo mazuri uwanjani.

Mchome amesema hayo baada ya Simba kukubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Tanzania Prisons juzi katika uwanja wa CCM Jamhuri mjini Morogoro.

“Mpira wa Tanzania hasa Simba wana imani sana za kishirikina na ndizo zinsababisha kupata haya matokeo mabovu. Tumecheza Azam Complex na TRA tulipata ushindi wa bao 6-0, unaogopa nini? Bila ushirkina huwezi kucheza?

“Waseme kama hawana pesa za kulipia Uwanja wa Chamazi, uwanja umetulia, unaweza kucheza hata usiku. Mfumo wa Simba tunacheza mpira wa pasi lakini tumechagua uwanja wa Jamhuri haurusu kupiga pasi, tunalazimika kupiga long balls.

“Uongozi uliopo Simba sio wa mpira, kama tatizo ni mapato hata Chamazi inaingiza mapato. Yanga inashinda uwanja wowote kwa sababu wachezaji wao wana ubora na wanajituma, ubora wa wachezaji wetu hawawezi kupambana kwenye uwanja kama ule. Hili suala waliondoe turudi Chamazi,” amesema Mchome.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: