Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchambuzi: Simba shida iko kwenye eneo la kiungo

Kanoute, Ngoma Mzamiru Viungo wa Simba SC

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msimu uliopita klabu ya Simba ilitengeneza muunganiko bora kwenye safu ya kiungo chini ya Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin na kuifanya ngome ya ulinzi ya Simba kutoruhusu mabao kirahisi.

Ujio wa Fabrice Ngoma kwenye kikosi umekuja kuondoa muunganiko wa Kanoute na Mzamiru na kupewa nafasi kubwa Fabrice ngoma kuanza na mmoja wao, Toka manadiliko hayo yamefanyika safu ya kiuongo cha Simba kimeshindwa kuwa imara,Timu inakosa uwezo wa kutawala mchezo katika kumilika mpira,Timu inakosa uwezo wa kujilinda kutokea eneo la kati na kupelekea lango la Simba kufikiwa kirahisi

Mimi ningetamani kuona kocha Robertinho kuanza kuwatumia viungo wote watatu katika mchezo dhidi ya Al Ahly, Kuwatumia Mzamiru na Kanoute katika kuitengeneza ballance timu kwenye kukaba na kulinda safu ya ulinzi, Ngoma kumpa uhuru wa kuichezesha timu kutokea nyuma kwaajili ya kuifanya klabu ya Simba mashambulizi yake yaundwe kutokea eneo lao la chini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: