Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbrazili Simba atenga saa 72 kutinga robo fainali ASFC

Fd Chama Kanoute Mbrazili Simba atenga saa 72 kutinga robo fainali ASFC

Fri, 7 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya mapumziko ya siku moja, kikosi cha Simba juzi Jumanne kilirejea kambini kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mchezo wao wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), huku kocha mkuu wa kikosi hicho akitenga saa 72 sawa na siku tatu kuipeleka timu hiyo nusu fainali.

Baada ya kipigo cha mabao 3-1 walichopata katika mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca, kikosi cha Simba kilirejea nchini Jumapili jioni ambapo licha ya kipigo hicho tayari wamefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali.

Simba Ijumaa hii wanatarajiwa kuvaana na Ihefu katika mchezo war obo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Akizungumza nasi, Meneja wa Habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema: “Baada ya mapumziko mafupi ya siku moja kikosi chetu kinatarajiwa kuingia kambini leo (juzi) Jumanne kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mchezo wetu wa robo fainali ya ASFC dhidi ya Ihefu.

“Tutakuwa na siku tatu za programu maalum ya kujiandaa na mchezo huo ambao tunaamini utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani, lakini tumejidhatiti kuibuka na ushindi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: