Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbrazil wa Simba apata dili jipya

Jefferson Luis Szerban.jpeg Aliyekuwa kipa wa Simba, Jefferson Luis 'Mbrazil' amepata dili jipya

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa kipa wa Simba, Jefferson Luis 'Mbrazil' amepata dili jipya baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja na timu ya Athletic Club ya nchini kwao.

Luis amesaini mkataba huo baada ya kupona majeraha ambayo aliyapata akiwa Simba hali iliyofanya avunjiwe mkataba.

Luis alisajiliwa na Simba ikiwa nchini Uturuki Julai mwaka huu kwa maandalizi ya msimu huu 'Pre-Seasson' ilitangaza kumsajili kipa Mbrazil ambaye hata hivyo hakumaliza hata wiki moja ndani ya kikosi hicho, akaachwa lakini sasa amepata timu.

Simba ilimpa mkataba wa miaka miwili, Jefferson lakini ililazimika kuvunja mkataba huo, baada ya nyanda huyo kuumia na kutarajiwa kupona baada ya miezi mitatu hadi minne.

Kiufupi Mbrazil huyo hakutua Bongo yalipo masikani ya Simba, aliishia Uturuki kambini tu kisha kurudi kwao Brazil kujiuguza.

Luis alisajiliwa na Simba ili kuziba pengo la Aishi Manula aliyekuwa majeruhi (Sasa amepona), lakini baada ya kuachana naye, Simba ilisajili makipa wawili kwa mpigo ikianza na Hussein Abel kutoka KMC na Mmorocco, Ayub Lakred ambao hata hivyo hawajaonyesha makali langoni kwa Mnyama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: