Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbrazil Simba aamue yeye tu

Robertinho Sersss Mbrazil Simba aamue yeye tu

Wed, 27 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Simba, Oliveira Roberto ‘Robertinho’ imeelezwa ana mastaa fundi wanaoweza kumpa kila kitu kinachotakiwa na jinsi ya kuwatumia kimbinu.

Simba haijapoteza mechi za mashindano kuanzia Ngao ya Jamii, Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ikishinda mabao 4-2, Dodoma Jiji mabao 2-0 na Coastal Union mabao 3-0 na Ligi ya Mabingwa Afrika ikitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Power Dynamos, lakini wadau wanaona kuna kitu cha zaida anachotakiwa kufanya kocha.

Winga wa zamani wa Simba SC, Steven Mapunda ‘Garrincha’ ameliambia Mwanaspoti jinsi ambavyo timu hiyo ilivyosajili majembe, lakini kazi ipo kwa kocha kuanza kuwatumia ili kupata mafanikio.

Alianza kutolea mfano kikosi ambacho alikipanga dhidi ya Power Dynamos.

“Mastaa waliingia kipindi cha pili dhidi ya Power Dynamos ambao ni Jean Baleke, Luis Miquissone, Said Ntibazonkiza ‘Saido’, Fabrice Ngoma bila kumsahau Moses Phiri anayehitaji mechi nyingi ili morali ya kufunga irejee,” alisema.

“Kikosi cha Simba kinahitaji muda kidogo huko mbele kitafanya vizuri, lakini itakuwa ngumu kama kocha ataendelea na aina ya upangaji mfano hao niliokutajia wapinzani wanapoona wachezaji kama hao wanakuwa na presha ya kupambana nao, hiyo inakuwa faida kwa Simba.”

Beki wa zamani wa timu hiyo, Boniface Pawasa alisema aina ya kikosi cha Simba ni mtihani kocha kuwatumia wote.

“Simba ina wachezaji wazuri sana licha ya kuhitaji muda wa kujuana na muunganiko mzuri. Pia kocha ana jukumu la kuhakikisha anamtumia kila mtu kucheza kwa kiwango, kwani cv zipo wazi ni wachezaji wanaojua mpira,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: