Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbivu na mbichi za Simba AFL kujulikana leo, upi utabiri wako?

Simba X Ahly 2 2.jpeg Mbivu na mbichi za Simba AFL kujulikana leo, upi utabiri wako?

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kitendo cha Simba kupata matokeo mazuri yatakayowavusha kuingia nusu fainali ya mashindano ya African Football League dhidi ya Al Ahly kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo,Misri leo kuanzia saa 11 jioni, sio tu yataifanya imalize unyonge dhidi ya Wamisri hao bali itawahakikishia kiasi cha Dola 1.7 milioni (Sh4.2 bilioni).

Simba inayohitaji ushindi wa aina yoyote au sare ya mabao kuanzia 3-3 ili isonge mbele, haijawahi kuitoa Al Ahly wala kupata ushindi dhidi yao wakiwa Misri katika shindano lolote walilowahi kukutana na hii itakuwa mara ya kwanza iwapo wakifanya hivyo.

Katika ardhi ya Msiri, Simba imekutana na Al Ahly mara tatu ambapo imepoteza zote pasipo kufunga bao hata moja huku ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara nane.

Na ikiingia nusu fainali, maana yake Simba itakuwa na uhakika wa kupata Dola 1.7 milioni (Sh4.2 bilioni) ambazo timu inayofika hapo ina uhakika wa kupata kutoka waandaaji wa mashindano hayo.

Simba inapaswa kuwa na nidhamu kubwa hasa ya kujilinda ili kuhakikisha Al Ahly hawana madhara makubwa kwao na wao waweze kupata matokeo mazuri yatakayowavusha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: