Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa watano Simba wapewa "Thank You"

Watemwa Simba yatema watano dirisha hili

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mastaa watano wa klabu ya Simba, wamepewa mkono wa kwaheri katika dirisha hili la usajili kupisha wachezaji wapya kutokana na kushindwa kufanya kile kilichotarajiwa na mashabiki wa timu hiyo.

Simba imeachana na mchezaji kiraka Nasoro Kapama, mshambuliaji Shaban Chilunda, kipa Ahmed Feruz, beki Jimmyson Mwanuke na kiungo Hamis Abdallah.

Chilunda na Abdallah ni wachezaji ambao walisajiliwa msimu huu na wameitumikia Simba kwa miezi sita kutokana na kushindwa kuonyesha kile kilichokuwa kinatarajiwa kutoka kwao, jambo ambalo limefana watupwe nje ya timu.

Wakati huo Mwanuke, Feruz na Kapama ni wachezaji ambao wamehudumu kwa muda ndani ya timu hiyo, lakini hawakuwahi kubahatika kupata namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya uongozi wa Simba kimeiambia Mwanaspoti kuwa uongozi umeamua kuchukua uamuzi huo kutokana na kocha mkuu, Abdelhak Benchikha kuhitaji kupunguza mrundikano wa wachezaji ndani ya timu.

"Kabla ya kufanya usajili mara baada ya kocha Benchikha kutupa ripoti amesisitiza kuwa na wachezaji wachache kikosini ambao watakuwa na mchango na kuondoa baadhi ambao hawana mchango," kilisema chanzo cheztu.

"Uamuzi tulioufanya ni sahihi na ni mpango ambao umefanyiwa kazi na benchi la ufundi, hivyo tunatarajia kabla ya dirisha kufungwa tutakuwa tumetimiza mahitaji ya benchi la ufundi."

Wakati Simba ikiwatema wachezaji hao tayari imewasajili Ladack Chasambi kutoka Mtibwa Sugar, kiungo Saleh Karabaka kutoka JKU na Babacar Sarr aliyewahi kucheza US Monastir ya Tunisia.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: