Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa walivyokwepa kikaango Simba

Mataa Kikosini Mastaa walivyokwepa kikaango Simba

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya mabosi wa Simba kuikabidhi timu kwa makocha Seleman Matola na Daniel Cadena inadaiwa benchi la ufundi limewaomba kuwarejesha wachezaji waliodaiwa kusimamishwa kikosini kwani timu inakabiliwa na mechi za Ligi Kuu pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Juzi, Simba iliachana na kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ikiwa ni siku mbili baada ya timu hiyo kufungwa mabao 5-1 na watani zao, Yanga kwenye mechi ya Ligi Kuu bara iliyochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Baada ya kuachana na kocha huyo kulikuwepo na taarifa za wachezaji sita kudaiwa kusimamishwa, lakini baadaye walirejeshwa kikosini na kwenda kujumuika mazoezini na wenzao.

Wachezaji hao walifanya mazoezi ya pamoja na wenzao ikiwa ni maandalizi ya mechi ya ligi dhidi ya Namungo FC itakayochezwa leo, Alhamisi kwenye uwanja huo.

Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo zinasema kuwa Matola na Cadena walifanya kikao na mabosi kuwataka wachezaji warudishwe kikosini hadi hapo baadaye uamuzi mwingine utakapofanyika.

“Ukiangalia waliotakiwa kusimamishwa wote ni tegemeo kikosini. Tuna mechi ngumu mbele yetu, hivyo makocha wamewaomba viongozi wawarudishe kikosini wachezaji ili wawe na kikosi kamili kuipambania timu halafu kama kuna adhabu ni baadaye.

“Kesho (leo) tunacheza na Namungo, kuna mechi dhidi ya Asec Mimosas mwezi huuhuu, zote tunahitaji kushinda, hivyo kama kuna matatizo kwa wachezaji hao basi viongozi wametakiwa kuyamaliza baada ya mechi hizi,” kilisema chanzo kutoka ndani ya timu hiyo.

“Pia benchi limeangalia kwamba kama (mabosi) wataruhusu wachezaji hao wakae pembeni hakutakuwepo na mbadala wao kwa sasa. Siyo rahisi, hivyo nadhani hiki kitu sasa kitafanyika Januari wakati timu ipo mapumziko na usajili wa dirisha dogo kama kuna ambao wataonekana hawafai, basi uongozi utaachana nao.”

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: