Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Simba wapewa siku 10

Simba SC BB.jpeg Mastaa Simba wapewa siku 10

Mon, 15 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Simba, Abdelhak Benchikha wamewapa mapumziko ya siku 10 wachezaji wake ambapo watarejea kambini Januari 24 mwaka huu, kujiandaa na mechi mbalimbali za mashindano wanayoshiriki.

Mapumziko ya wachezaji hao yameanza mara baada ya kurejea kutoka kisiwani Zanzibar, ambako timu hiyo ilikuwa inashiriki mashindano ya Kombe la Mapinduzi.

Katika mashindano hayo, Simba ilikuwa mshindi wa pili huku Mlandege ikitetea kombe hilo kwa ushindi wa bao 1-0, mchezo uliochezwa juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Amaan Complex, Unguja.

Simba ikirudi kambini itakuwa na kibarua cha kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara, Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi pamoja na mechi ya Kombe la Shirikisho la Azam.

Miongoni mwa mechi ambazo huenda Simba ikaanza nazo ligi itakaporejea baada ya kumalizika kwa michuano ya Afcon inayoendelea nchini Ivory Coast ni zile za viporo dhidi ya Azam FC, Mashujaa na Geita Gold FC.

Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally alisema wachezaji wamepewa mapumziko kwa siku hizo kwani wamekuwa katika majukumu ya timu kwa muda mrefu.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: