Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki wa Simba acheni visingizio

Ihefu Msh(1) Mashabiki wa Simba acheni visingizio

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kumeibuka mjadala kwa baadhi ya mashabiki wa Simba wakidai kuwa Yanga inashinda mechi nyingi kwa vile mdhamini wao wambaye ni GSM kupitia mwamvuli wa Kampuni zake Tanzu ana dhamini timu nyingine za Ligi Kuu Bara hivyo kuna conflict of interest ambayo Yanga kwa namna flani wanaweza kuwa wananufaika.

Baada ya Simba SC kupoteza dhidi ya Prisons (1-2) na kushinda kwa mbinde (1-2) dhidi ya Coastal, imeibuliwa hoja DHAIFU sana na baadhi ya Maashabiki maarufu wa Simba SC mitandaoni na baadhi ya wachambuzi kwenye Media.

Wanasema kuwa kampuni ya HAIER inayozidhamini klabu za Yanga, Ihefu, Namungo na Coastal Union inaisaidia Yanga kushinda mechi zake kwa kile wanachodai kuna (Conflict of interest) uwezekano wa kupanga matokeo na kuzipa motisha timu zinazocheza na Simba ili ziwakamie.

Awali baada ya kuona hoja hizi nilizipuuza kwa sababu zimetolewa na mashabiki. Kitu kilichonishtua ni kuona baadhi ya wachambuzi wanaoaminika kuaminisha watu kuwa kinachosemwa kina mashiko.

Hebu nisikilizeni

Kwanza kabisa hakuna kanuni au sheria Duniani kote iliyo chini ya (FIFA) au (CAF) inayokataza kampuni moja kudhamini vilabu tofauti katika ligi moja. Badala ya kufurahia vilabu vyetu kupata udhamini unaozisaidia timu hizo sisi tunataka kuwakatisha tamaa wadhamini ambao tuliwalilia waje kwenye soka letu kwa miaka mingi.

(FIFA) inazuia vilabu zaidi ya kimoja kumilikiwa na kampuni / mtu mmoja kwenye ligi moja, haizuii UDHAMINI (SPONSORSHIP). FIFA wanapinga kampuni moja kumiliki vilabu zaidi ya kimoja hawana shida kabisa kwa kampuni 1 kuvidhamini vilabu tofauti hata viwe (100).

Pili, hili suala la kampuni moja kudhamini timu tofauti katika ligi moja Tanzanua halijaanza leo, limeanza misimu kadhaa iliyopita kwa nini hoja hizi zinaibuka sasa ?

Misimu (3) iliyopita kampuni ya METL inayomilikiwa na MOHAMED DEWJI ilikuwa inaidhamini klabu ya Lipuli na baadae Namungo FC kupitia sabuni ya MO POA, wakati huohuo METL ilikuwa inaidhamini Simba SC na sio kuidhamini pekee bali mmiliki wa kampuni ya METL Mo Dewji ni sehemu ya umiliki wa klabu ya Simba SC akiwa na hisa 49%... Kwa nini hoja hizi hazikuwepo?

Kabla ya Mohamed Dewji kununua hisa Simba SC alikuwa mmiliki wa klabu ya African Lyon, wakati huohuo akiwa mfadhili wa klabu ya Singida Utd,, hoja hizo mbona hazikuibuliwa iwe sasa?

Nataka kuuliza tu kwamba, Bakhresa kupitia Azam TV anadhamini vilabu vyote vya Ligi Kuu ya (NBC) na wakati huohuo ana timu ligi kuu (NBC) inaitwa AZAM FC, vipi hapa hakuna Conflict of interest?

(DSTV) wanazidhamini klabu zote za ligi kuu ya South Africa lakini pia wana timu kwenye ligi hiyohiyo iitwayo Supersport,. hawa nao hawana fair competition?

Vipi kuhusu Vunjabei, Binslum na Sportpesa kuzidhamini timu zaidi ya 1 kwenye ligi 1 au tumekula Ganja mbichi tumesahau?

Simba SC - Vunjabei.

Prisons - Vunjabei

Polisi Tanzania - Vunjabei

Singida FG - Vunjabei

Coastal Union - Binslum Tyres

Stand utd - Binslum.

Mbeya City - RB Binslum Battery

Ndanda - Binslum Vee rubber

Simba SC - Sportpesa

Young Africans - Sportpesa

Singida FG - Sportpesa

Namungo - Sportpesa

Tatu, Yanga msimu huu mpaka sasa ameshinda mechi 15 kati ya 17, katika mechi alizoshinda kuna timu mbili tu zinazodhaminiwa na HAIER, kama ingekuwa hivyo basi hizi timu zinazodhaminiwa na HAIER angezifunga (10-0), lakini hizi ndizo timu zilizompa mechi ngumu zaidi Yanga.

1 - 0 Coastal Union.

1 - 0 Namungo.

1 - 2 Ihefu FC ✖️

3 - 1 Namungo

Baadhi ya timu ambazo hazidhaminiwi na HAIER zilizokutana na Yanga msimu huu ,;

5 - 0 KMC

5 - 0 JKT Tanzania

5 - 1 Simba SC

4 - 1 Mtibwa sugar

3 - 2 Azam FC

3 - 0 Geita gold

3 - 0 KMC

Kwa hiyo na timu hizi zinadhaminiwa na HAIER? Kwamba ni tawi la Yanga zinapanga matokeo ndio maana zinapigwa tano tano?

Hebu tutengenezeni timu zetu, tuache kuaminishana Ujinga. Kutokukubali Ubora wa Yanga kwa sasa ni kuwarahisishia Yanga kutwaa UBINGWA watakavyo.

Siku tutakapokubali ubora wao ndio siku tutajua njia ya KUWAZUIA kuchukua makombe, vingine ni maneno ya mkosaji tu.

Kwani HAIER anazidhamini klabu huko (CAF)? Yanga Sc wamewezaje sasa kufika fainali CAFCC na robo fainali CAFCL? Mashabiki wa Simba acheni visingizio.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: