Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki Yanga wazipongeza Simba, Azam usajili wa kibabe!

Rfg Simba Ngoma Malone Mashabiki Yanga wazipongeza Simba, Azam usajili wa kibabe!

Sun, 16 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kumbe mashabiki wa Yanga wanaufuatilia kwa karibu usajili wa wapinzani wao wakubwa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Simba na Azam na kuwapa tano kwa majembe waliyoyashusha, huku wakiwatisha kwamba bado hawajafua dafu kwa kilichofanywa na Yanga kwani nyota anayesubiriwa kwa hamu kubwa ‘namba 6’ amezua hofu kwa majirani.

Yanga imewasajili Max Nzengeli, Nickson Kibabage, Kouassi Yao, Jonas Mkude na Gift Fred, huku Simba ikiwanasa Fabrice Ngoma, Willy Onana, Che Fondoh Malone, David Kameta ‘Duchu’ na Kramo Aubin wakati Azam imewashusha Cheikh Sidibe, Alassane Diao, Feisal Salum na Djibril Sillah.

Mwanachama na shabiki lialia wa Yanga jijini Mwanza, Haruni Popat amesema usajili huo utaleta ushindani mkubwa, ladha na kunogesha Ligi Kuu bara lakini akatamba kuwa klabu yao imefanya usajili makini zaidi akiamini ‘namba sita’ wao amewafanya watani wao kuingiwa na ubaridi.

“Msimu huu klabu yetu tumesajili wachezaji wa gharama kubwa na wanatoka timu zao za taifa wana uwezo wa kuleta changamoto na kitu kipya katika klabu yetu, nawapongeza pia Simba na Azam kwa kufanya usajili ambao utaleta ushindani katika ligi yetu,”

“Naona msimu huu ligi itakuwa ngumu kweli sasa mbinu za makocha ndizo zitaamua nani awe bingwa na anastahili kushinda, wachezaji wazawa wana uwezo mkubwa wa kupambana na kuonyesha ushindani na kuifanya ligi yetu kuwa bora,” amesema

Baada ya kufanikisha uzinduzi wa ‘Wiki ya Mwananchi’ kitaifa katika Uwanja wa Furahisha, Mwenyekiti wa Yanga tawi la Mwanza Mjini, Salehe Akida amesema hatua ya uongozi wa klabu hiyo kuleta jambo hilo jijini humo ni la kupongezwa huku akiomba kilele cha tamasha msimu ujao kifanyike Mwanza.

“Ni fursa adhibu kwa mkoa wetu kupewa shughuli hii siku zote Mwanza haijawahi kufeli tulitamani kilele cha tamasha hili kiwe Mwanza, kila kitu kina mwanzo tumeonesha inawezekana tunaamini tulichokifanya leo itakuwa fursa tosha kuletewa kilele hapa inshallah wakati mwingine tutaletewa,” amesema Akida na kuongeza

“Kutakuwa na magari ya kupeleka mashabiki Dar es Salaam kwenye kilele kunogesha sherehe tutaondoka Julai 20, mwaka huu kwahiyo Wana Yanga kote Kanda ya Ziwa safari itakuwepo nauli ni Sh70,000 kwenda na kurudi. Pia Jumatano tutakuwa na tukio la uchangiaji damu salama kila tawi lilipo kwenye kata yao wakusanye watu wao kwenda kuchangia damu,”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: