Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashabiki Simba wamtaka Manula leo

Walinda Milango Simba.jpeg Mashabiki Simba wamtaka Manula leo

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baadhi ya mashabiki wa wekundu wa Msimbazi Simba wameonekana kuimisi huduma ya mlinda mlango wao namba moja Aishi Manula 'Tanzania One' katika mchezo wa leo dhidi ya Al Ahly.

Simba saa 12 jioni ya leo itakuwa dimbani kuzipigania dakika 90 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam ikiwa ni ufunguzi wa michuano ya African Football League ambayo inashirikisha timu nane bora Afrika.

Baada ya Simba kuposti tangazo linalomuonyesha Manula na Jean Baleke mashabiki hawakusita na kuonyesha namna ambavyo wamemis Manula na kutamani kumuona leo.

Mariam Thomas amesema amefarijika kuona Manula amepona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua hivyo kama yuko fiti apewe nafasi katika mchezo mgumu wa leo.

"Kama Manula amepona naomba aanze tu jamani, maana yule mwarabu mmmmm,"ameandika mwanasimba huyo.

Huku Faraji Abdallah akisema, "Nina imani na wachezaji wetu lakini akianza Manula roho zetu zitatulia, walau hata Salim lakini yule Mwarabu presha zinakuwa kubwa mtatuua," amesema Faraji

Aquila Shaibu amesema "Hatima ya ushindi wa Mnyama iko mikononi mwa kikosi ambacho kocha atakipanga kwa umairi wa Manula naamini tutawashangaza wengi," amesema

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: