Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marumo waipiga changa la macho Yanga

Marumo Gallants Er Marumo waipiga changa la macho Yanga

Tue, 9 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Marumo Gallants kutoka Afrika Kusini ambayo itachuana na Yanga kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza kombe la Shirikisho barani Afrika bado haijafanya mawasiliano na wenyeji wake, Klabu ya Yanga.

Kwa mujibu wa kanuni za CAF, Yanga ikiwa mwenyeji wa mchezo huo ina jukumu la kuwapokea wageni wao na kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu ikiwa ni pamoja na kuwapa usafiri kutoka uwanja wa Ndege mpaka hoteli watakayofikia

Afisa habari wa Yanga Ally Kamwe amesema klabu imefanya jitihada muhimu za kuwasiliana ma Marumo lakini hawajajibu wala kutoa taarifa juu ya ujio wao

Hata hivyo Kamwe amesema wanazo taarifa ambazo sio rasmi kuwa klabu hiyo huenda ikawasili nchini mapema Jumanne ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo dhidi ya Yanga

"Ni kweli hatuna taarifa za ujio wa Marumo Gallants. Tuliwaandikia barua kuuliza wanakuja lini Tanzania hili ni jambo la kikanuni kabisa lakini hawakujibu hivyo mpaka sasa hatujui wanakuja lini. Ila za ndani kabisa baada ya kufanya research yetu tumebaini watakuja kesho (leo) asubuhi.

"Kwa mujibu kanuni za Shirikisho la Soka Afrika (CAF), sisi kama wenyeji tuliwaandikia barua Marumo Gallants kuwauliza wanakuja lini, lakini hawakujibu, lakini hawakujibu na mpaka sasa hatujui wanakuja lini.

Lakini za ndani kabisa tulizozinyaka ni kwamba wanafika kesho (leo) asubuhi. Hili ni jambo la kikanuni, kwa hiyo kama hawajatoa taarifa kwenu watapigwa faini ya dola 4,000, CAF wamenyooka kama rula.

"Huu sio ujanja bali ni kuitia hasara klabu, sisi tunaamini ubora ndani ya uwanja ndio utaamua nani atashinda na si mipango ya nje ya uwanja. Yanga sisi tumejikita kwenye pitch, morali ipo juu na maandalizi yako vizuri Avic Town. Wachezaji wanataka kuweka historia," alisema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: