Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manula apewe 'Thank You' na Simba

Manula X Cadena Shabiki Simba: Manula aondoke Simba

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki kindakindaki wa Simba SC, Mchome Mapovu amesema kuwa kipa wa timu hiyo, Aishi Manula amechoka na hana uwezo tena wa kuendelea kuitumikia timu hiyo kama zamani.

Mchome amesema hayo baada ya Simba kukubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Tanzania Prisons juzi katika uwanja wa CCM Jamhuri mjini Morogoro.

“Pale Simba kipa aliyebaki ni Ayoub Lakred peke yake. Aishi Manula ukiangalia tangu AFCON mabao aliyofungwa utashangaa. Sisi tuna wachezaji wa historia, kwamba alifanya nini misimu mitatu mine nyuma. Manula tayari kiwango chake kimeisha.

“Bao la kwanza Mbangula alijitangulizia ule mpira, Manula alikuwa na uwezo wa kwenda kupunguza lile gape na kumsumbua mshambuliaji yule, lakini akaganda golini, akili inataka ila mwili hautaki.

“Manula ukimwangalia hata muonekano wake unaona umri umeenda, amechoka. Itoshe kusema Manula ameshafanya mambo mengi sana Simba, tumpe asante ili tuwape nafasi makipa wengine waoneshe uwezo wao. Manula akidaka tunshikilia roho mkononi, Aishi Manula kiwango kimeisha,” amesema Mchome.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: