Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara: Barbara alivyoteuliwa Simba niliomba kuacha kazi

MANARA Manara: Barbara alivyoteuliwa Simba niliomba kuondoka

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyewahi kuwa msemaji wakLabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa baada kuteuliwa jwa barbara Gonzalez kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo, yeye alimpigia simu Mohammed Dewji na kuomba aondoke.

Manara amesema alifanya hivyo kwa sababu alijua fika kuwa hatoweza kufanya kazi na dada huyo kutokana na tabia zake.

“Simba walikuwa wananilipa mshahara usiokuwa na mkataba maalumu, Yanga wamemiwekea mzigo mezani, mapenzi ya mashabiki wa Yanga ni makubwa kuliko yale ya Simba sasa kwanini hiyo timu mimi nisiipende.

“Barbara wakati anateuliwa kuwa mjumbe wa bodi, wakati huo CEO wetu alikuwa Senzo na Senzo alikosa raha kwa sababu ya kuingiliwa majukumu yake, baadae Senzo akaenda Yanga, Barbara akawa CEO na mimi nilishaona huyu hatuwezi kufanya kazi pamoja.

“Alivyoteuliwa tu nikampigia simu Dewji kumueleza kwamba nataka kuacha kazi, siwezi kufanya kazi na Barbara tutagombana, wakatuitishia vikao zaidi ya saba, kuna siku uongozi ukasema umeshindwa na wote wanatuhitaji kakaeni wenyewe.

“Nilikaa kikao na Barbara toka saa 10 jioni mpaka saa 7 usiku, shida kubwa Barbara aliingia pale na kutaka kuonyesha power yangu ni ndogo,” amesema Manara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: