Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malone sio mtu sahihi kuziba nafasi ya Onyango - Ngereza

Malone Che Che Fondoh Malone

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Alex Ngereza ameuponda usajili wa beki wa kati walioufanya Simba SC wa kumvuta Che Fondoh Malone kutoka Cameroon ambaye amekuja kuchukua nafasi ya Joash Onyango.

Akizungumzia usajili huyo, Ngereza amesema kuwa; "Simba wamepewa presha tu na mashabiki lakini Malone hakuwa mtu sahihi wa kuja kuchukua nafasi ya Onyango, ukiangalia timu aliyotoka Malone sio timu kubwa na wala kiwango cha Malone sio kikubwa kiasi hicho ambacho watu wanatarajia."

Baada ya kutoa kauli hiyo, mdau mwingine wa michezo (jina tunalo), ameibuka na kujibu hoja hiyo akisema;

"Tanzania ni nchi pekee ambayo watu wake wanamjua kila mtu Duniani, bahati mbaya zaidi hao wajuzi wa mambo wanajua mpaka kesho za wenzao.

"Ungemuuliza huyu kabla Yanga hawajamsajili Ibrahim Bacca kwamba Bacca anastahili kucheza Yanga angesema sio mtu sahihi kwa sababu anatoka timu ndogo.

"Namkumbusha, Dickson Job alitoka Mtibwa Sugar akachukua namba ya Lamine Moro, Gael Bigirimana alicheza EPL ila kashindwa kucheza Bongo," amesema mdau huyo.

Nini maoni yako?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: