Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makocha Mashujaa, Simba uso kwa uso

Benchikha Saikolojia.png Makocha Mashujaa, Simba uso kwa uso

Fri, 2 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara inatarajia kuendelea kesho katika Uwanja wa Lake Tanganyika, mjini Kigoma na Mashujaa Fc itakuwa mwenyeji wa mchezo huo kwa kuwakaribisha Simba.

Kocha wa Mashujaa FC, Abdallah Mohammed 'Barres' amesema mchezo ni muhimu kwao kwani wamejipanga kupata alama tatu licha ya kuwa wanacheza na klabu bora na kubwa ligi kuu.

Omary Kindamba amesema wachezaji wana hali na morali ya kutosha na hivyo amewataka mashabiki wao kujaa kwa wingi na kuisapoti timu yao kutokana na maandalizi waliyofanya wakati ligi hiyo wakati imesimama.

Kwa upande Simba. Kocha Msaidi wa timu hiyo, Seleman Matola amesema anajua Mashujaa wamejipanga kupambana ili wapande juu kwenye msimamo, pamoja na ugumu wa mechi watahakikisha kesho wanapata matokeo mazuri.

“Tunajua wamejipanga kupambana kutafuta pointi tatu ili wapande juu kwenye msimamo pamoja na ugumu wa mechi hiyo tutapambana kupata alama tatu ambazo ni muhimu kwetu na kwenda kwenye mechi inayofuata dhidi ya Tabora United,” amesema.

Amesema Mashujaa imefanya usajili mzuri wa wachezaji wake hivyo mchezo huo utakuwa sio rahisi kama wanavyofikiria lakini pamoja na hivo watahakikisha wanatoka na ushindi katika dimba la Lake Tanganyika.

Mchezaji wa Simba, Israel Mwenda amesema kutokana na mapokezi waliyoyapata mkoani humo kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo kitu pekee ambacho wanawahidi ni kupata ushindi dhidi ya Mashujaa FC.

Amesema unapokwenda ugenini na ukapokewa vizuri na mashabiki, hali hiyo inakupa nguvu na motisha ya kufanya vizuri katika mchezo, hivyo wanatarajia mashabiki kujitokeza kwa wingi.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: