Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabao mawili yambeba Kanoute AFL

Sadio Kanoute Second Goal.jpeg Mabao mawili yambeba Kanoute AFL

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo mkabaji wa Simba, Sadio Kanoute ni miongoni mwa wachezaji wanne waliomaliza kama vinara wa mabao kwenye michuano mipya ya African Football League (AFL) iliyomalizika jioni ya leo Jumapili.

Mamelodi Sundwons ya Afrika Kusini ndio iliyofanikiwa kuwa mabingwa wa kwanza wa michuano hiyo kwa kuilaza Wydad CA ya Morocco kwa mabao 2-0 katika mechi ya pili ya fainali, iliyopigwa jijini Pretoria, Afrika Kusini.

Kanoute kama ilivyo kwa wachezaji wengine watatu akiwamo Oussema Bouguerra wa Esperance ya Tunisia, Kahraba wa Al Ahly ya Misri na Thapelo Maseko wa Mamelodi Sundowns, amefunga mabao mawili, yote yakiwa ni dhidi ya Al Ahly iliyowang'oa Wekundu hao kwenye hatua ya robo fainali.

Maseko ndiye aliyekabidhiwa tuzo hiyo ya Mfungaji Bora na ya Mchezaji wa michuano hiyo.

Kiungo huyo raia wa Mali alifunga bao moja wakati Simba ikilazimisha sare ya 2-2 nyumbani na kufunga jingine jijini Cairo katika sare ya 1-1, lakini Wekundu wakang'olewa kwa sheria ya bao la ugenini baada ya matokeo ya jumla kuwa sare ya 3-3 na Al Ahly ikaingia nusu fainali iliyong'olewa na Mamelodi.

Nyota hao wanne wenye mabao mawili wanawaongoza wachezaji wengine 15 waliofunga bao moja kila mmoja akiwamo nyota mwingine wa Simba, Kibu Denis.

Michuano hiyo iliyozinduliwa msimu huu ilishirikisha jumla ya timu nane, zikiwamo TP Mazembe ya DR Congo, Enyimba United ya Nigeria, Petrro Atletico du Luanda ya Angola na Wydad Casablanca ya Morocco ilifungwa jioni hii mabao 2-0 na Mamelodi kwenye mechi ya pili ya fainali iliyopigwa Afrika Kusini baada ya awali kulala 2-1 ugenini jijini Casablanca, Morocco wiki iliyopita.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: