Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Luis: Tulieni, miguu itaongea

Miquissone Tik.jpeg Luis: Tulieni, miguu itaongea

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Simba inaendelea kujifua kujiandaa na mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ya Zambia, huku nyota wawili wa timu hiyo, Luis Miquissone na Fabrice Ngoma wakianza kujipata kiasi cha kumkuna kocha, lakini Luis amewataka mashabiki watulie, kwani miguu itaongea.

Wekundu hao wataikaribisha Dynamos katika mechi itakayopigwa Oktoba Mosi kwenye Uwanja wa Azam Complex, baada ya awali kutoka sare ya 2-2 mjini Ndola, lakini viwango vya Ngoma na Luis zimemfanya Kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ kukiri mambo kwa sasa ni moto na wapo tayari kuwavaa Wazambia.

Nyota hao wawili hao walisajiliwa na Simba msimu huu, Luis akirejea baada ya kuitumikia kwa misimu miwili na kuuzwa Al Ahly ya Misri msimu wa 2021/2022, wakati Ngoma ametua akitokea Al Hilal ya Sudan.

Kocha Robertinho alikaririwa juzi akisema kwamba anafurahishwa kurejea kwenye ubora kwa wachezaji hao na hasa Luis, kwani anaamini sasa atawapa raha mashabiki wa klabu hiyo waliokuwa wana hamu ya kuona ile kasi aliyokuwa nayo kabla ya kuuzwa Al Ahly.

Hata hivyo, akizungumza na Mwanaspoti winga huyo kutoka Msumbiji aliyesajiliwa na Simba kutoka UD Songo baada ya kuwapiga bao tamu lililowang’oa Wekundu wa Msimbazi kwenye raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2019-2020, alisema hana maneno mengi na badala yake akaahidi kuiacha miguu yake iziungumze zaidi.

Luis aliyesababisha penalti iliyowekwa kimiani na Jean Baleke na kukamilisha hat trick kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, alisema kwa muda ambao tangu ajiunge na timu hiyo na kutokuwa fiti alikuwa akizingatia vyema programu za mazoezi alizopewa na wataalamu wa benchi la ufundi na sasa yupo tayari kwa kazi ya kuipigania Simba kwa nguvu zote.

“Nilihitaji muda kidogo kuzoea na kurejea kwenye ubora, nilikuwa nikifanya mazoezi kwa nguvu nikifuata programu kutoka kwa wataalamu wa timu pia juhudi binafsi. Sasa kila kitu kimebadilika na nipo tayari kupambana zaidi, sitaki kuongea sana nadhani vitendo vitaonekana uwanjani,” alisema Luis.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: