Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lakred alegeza uzi Msimbazi, Manula kazi anayo

Lakred X Manula Lakred alegeza uzi Msimbazi, Manula kazi anayo

Thu, 30 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba SC imefanya kikao kizito cha kumshawishi Golikipa wake raia wa Morocco Ayoub Lakred abadili maamuzi yake ya kuondoka ndani ya Klabu hiyo.

Mazungumzo baina ya pande hizo mbili yameonekana kuwa na mwanga na ofa watakayompa ni ya mkataba miaka miwili.

Kuna vitu vichache vinamaliziwa kisha atasaini mkataba mpya. Walati Ayoub akiwa katika nafasi nzuri ya kuvaa jezi ya Simba msimu ujao, Klabu hiyo pia vile vile imehusishwa kumuhitaji Golikipa wa Coastal Union Ley Matampi.

Uwepo wa Ayoub unaleta changamoto kwa Golikipa Mkongwe Aishi Manula ambae amekuwa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha huku Lakred akionesha kiwango safi katika michezo aliyocheza.

Kwa kifupi kazini kwa Manula kuna kazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: