Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa usajili huu, Simba tunarudisha makombe yote - Mchachu

Simba Day One.jpeg Kwa usajili huu, Simba tunarudisha makombe yote

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki kindakindaki wa Klabu ya Simba, Mzee Chachu amesema kuwa kutokana na usajili mzuri walioufanya klabu hiyo msimu huu anamaanini watakuchua vikombe vyote ambavyo kwa sasa anavishikilia mpinzani wao Yanga Sc.

Mchachu amesema hayo wakati akizungumza na chombo kimoja cha habari kutoa tathmini yake kuelekea msimu ujao baada ya timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC kufanya usajili.

"Usajili wetu msimu huu ni bab’kubwa, tumesajili kama tulivyokuwa tunahitaji, mfadhili wetu Mo Dewji ameitika, usajili wetu mzuri sana tena sana labda yatokee mambo mengine kwa maana huu mpra bana huwezi kujua.

"Lakini nasema safari hii Mungu akitujalia tunarudisha vikombe vyetu vyote, na klabu Bingwa Afrika makundi ni lazima kama kawaida.

"Kurejea kwa Luis Miquissone kutaongeza nguvu Simba kama mpira wake utakuwa ule ule wa miaka mitatu nyuma (alivyokuwa Simba kabla ya kuondoka). Nasema mwaka huu ni moto wa kuotea mbali.

"Huko beki yenyewe kuna Mcameroon (Che Fondoh), Mkondo (Inonga), kipa mwenyewe Mbrazil sio yule wa Yanga anadaka mishale huyu anadaka mipira saba kwenye goli. Kocha Brazil na kipa Brazil mwaka huu ni hatari.

"Kusema kwamba tumepigwa ni jambo la kawaida kwenye utani wa jadi lakini hata wao wameleta mchezaji anacheza Amapiano, mchezaji anarusha mipira kwenye mikono! Haya, hii sio ligi ya Sauzi ni Ligi ya Bongo kama Uingereza," amesema Mzee Mchachu.

Simba imeongeza nguvu kwenye upande wa usajili ambapo mbali na Luis ambaye ni kipa ameungana na nyota wengine wapya ambao ni Willy Onana, Che Malone Fondoh, Aubin Kramo, Fabrice Ngoma.

Pia, yupo kiungo Luis Miqussone, David Kameta wengi hupenda kumuita Duchu, Hamiss Abdallah, Hussein Kazi na Shaaban Chilunda hawa kuanzia kwa Duchu ni wazawa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: