Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa hili Simba wapewe maua yao

F8ZCOdbWkAA5wr .jpeg Kwa hili Simba wapewe maua yao

Sat, 14 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba kila inapokaribia kushiriki katika matukio makubwa imekuwa na kasumba ya kulipeleka jambo lao moja kwa moja kwa mashabiki wake ambao ndio wenye timu ambalo ni jambo zuri sana.

Katika matukio yaliyopita walifanya matamasha mbalimbali lakini kuelekea mchezo wa ufunguzi wa African Football League wameamua kuanzisha Bonanza la mpira wa miguu linalohusisha matawi yao.

Hii inaongeza thamani zaidi kwa klabu na mashabiki kupenda kujiunga na matawi na waliopo kuwa "Active" ili washiriki moja kwa moja kwenye matukio ya klabu yao.

Leo wamezindua Bonanza la Beach rasmi na timu za matawi nyingi zimeshiriki, msafara kuelekea kwenye uzinduzi umeanzia kwenye makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya msimbazi kuelekea beach ambapo ndio Bonanza hili linafanyika.

Hili linaenda kuongeza hamasa na thamani maradufu kuelekea mchezo wao dhidi ya Al Ahly, na sasa itazungumzwa Simba tu na wapenzi na mashabiki wa soka.

Kudos kwa ubunifu huu, Simba wapewe maua yao kwa hili, nafurahi timu kuziona zikishindana kwenye ubunifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: