Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kubeza mashindano ya AFL ni ushamba

Walinda Milango Simba.jpeg Kubeza mashindano ya AFL ni ushamba

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Hakuna sababu ya kuyabeza mashindano ya African Football League (AFL) kama ambavyo baadhi ya mashabiki hoyahoya wanafanya hivi sasa.

Unayabeza vipi mashindano ambayo kwanza uzinduzi wake unafanyika nchini mwako na dunia nzima itaelekeza macho, masikio na akili hapa kutokana na ukubwa wa tukio lenyewe na wageni watakaokuja?

Kwa kufanyika tu uzinduzi wake hapa, kuna fursa nyingi ambazo nchi na hata mtu mmojammoja anaweza kupata kuanzia zile za kisoka, kiuchumi na hata kijamii.

Tanzania kufuatiliwa kwa ukaribu, kunatengeneza fursa katika sekta ya utalii ambayo ni miongoni mwa nyanja tegemeo za uchumi wetu na pia imekuwa ikisaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza fedha za kigeni hapa nchini.

Lakini ukarabati mkubwa wa Uwanja wa Benjamin Mkapa ambao umefanyika kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo, hautoihusu Simba tu kwani kuna timu nyingine za hapa nyumbani baadaye zitakuja kucheza kwenye uwanja huo ambao ndio unaoongoza kwa ubora na kuingiza idadi kubwa ya mashabiki hapa nchini kuliko mwingine wowote.

Mashindano hayo kuzinduliwa hapa nchini ni fursa ya kupata uzoefu mpya wa masuala ya kisoka ukizingatia kuna idadi kubwa ya wadau wakubwa wa soka kutoka maeneo mbalimbali duniani ambao wapo hapa kushuhudia uzinduzi wake kutokana na mwaliko wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (Fifa) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf).

Kuna ugeni wa watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 450 ambao umekuja hapa nchini na katika muda watakaokuwepo kuna uingizaji mkubwa wa kipato.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: