Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kramo nje tena Simba

Aubin Kramo Manula Kramo nje tena Simba

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinda mlango wa wa klabu ya Simba Sc, Aishi Manula 'Air Manula' na winga Aubin Kramo hawatakuwa sehemu ya kikosi ambacho kitakipiga kwenye mchezo wa marudiano wa michuano ya African Football League dhidi ya Miamba ya Misri na Afrika Al Ahly.

Manula ameshapona majeraha yake lakini hayupo fiti kimchezo japo kuwa ameshaanza mazoezi na wachezaji wenzake huku Kramo bado yupo nchini kwao ambapo alienda kuuguza majeraha yake yaliyokuwa yanamsumbua.

Kwenye orodha ya wachezaji 24 waliosafiri kuelekea nchini Misri majina ya Aishi Manula na Aubin Kramo hayapo hii inaashiria kutokuwepo kabisa kwenye mchezo huo unaotarajiwa kupigwa Oktoba 24 katika dimba la Cairo International.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: