Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kramo ndiyo usajili Bora walioufanya Simba msimu huu

Aubin Kramo Nje Kramo ndiyo usajili Bora walioufanya Simba msimu huu

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aubin Kramo Kouamé(28) ni miongoni mwa majina ambayo msimu huu wa mashindano unaomalizika mashabiki wa Simba na wadau wengi wa soka walitamani kumuona uwanjani, watu walitaka kuona ni kitu gani cha tofauti atapeleka ndani ya Msimbazi hasa katika eneo la ubunifu ambalo Timu inahitaji wachezaji wengi ili kuzalisha idadi kubwa ya magoli

Pale Ligi Kuu ya Ivory Coast ukitaja jina la Aubin Kramo basi utakuwa umetaja miongoni mwa majina ya wachezaji wachache sana wenye vipaji vikubwa sana ambao wamepita ndani ya Ligi hiyo, pale wamtambua Aubin Kramo kama mchezaji ambaye alipaswa kuwa kwenye orodha ya wachezaji ambao wapo Ulaya kama Karim Konate, Sankara Kalamoko na wengineo waliotoka pale

Kama ambavyo Stephane Aziz Ki na Pacome Zouzoua walikuwa MVP wa Ligi Kuu ya Ivory Coast basi Aubin Kramo alifanya hivyo pia kwa Msimu wa Mwaka 2022-23, Kramo wakati anaingia Simba aliingia kama MVP wa Ligi Kuu y Ivory Coast na katika wakati ambao watu wanatamani kuona miguu yake inaleta kitu gani ndani ya uwanja basi ndio wakati ambao anapata majeraha.

Majeraha ambayo amepata Aubin Kramo muda mwingi yamemuweka nje ya uwanja na Msimu huu unamalizika ikiwa Simba SC haijaona hata Robo ya Ubora wake aliotoka nao ndani ya Ivory Coast akiwa kama MVP.

Hapa ukiacha Benchi jipya la Ufundi, Utamaduni, Ada ya Usajili, Wachezaji anaowakuta mchezaji husika na vitu vingine basi majeraha pia ni miongoni mwa vitu ambavyo hufanya mchezaji aonekane amefeli ndani ya Timu fulani.

Binafsi bado naamini kama ambavyo nilishasema hapo awali AUBIN KRAMO KOUAMÉ ndio Usajili Bora ambao Simba walifanya katika Dirisha kubwa la Usajili lililopita ni vile majeraha yamefanya amekuwa nje muda mwingi kuliko uwanjani, kama Simba ingepata hata Robo Tatu ya Ubora wake ambao alitoa ndani ya Asec Mimosas basi kuna sehemu kubwa sana wangesogea kutokana na uwezo alionao.

Simply! Mkataba wa Aubin Kramo unamalizika June 30 Mwaka 2025 na Kwakuwa Msimu mpya unaanza hivi karibuni basi tusubiri ataleta kitu gani ndani ya uwanja, pia kama yupo vizuri kurejea uwanjani na Simba wakabaki naye huenda basi wakapata kitu bora sana ambacho walihitaji kutoka kwenye ubongo na miguu yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: