Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kramo jukwaani Kwa Mkapa

Kramo Fiti(2) Kramo jukwaani Kwa Mkapa

Fri, 29 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Winga wa Simba asiyetumika kwenye mechi za timu hiyo, Aubin Kramo ametinga jukwaa la Wanahabari ili kushuhudia pambano wa kikosi hicho dhidi ya Al Ahly ya Misri linalopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa usiku huu.

Muivory Coast huyo ambaye tangu asajiliwe Simba msimu huu, hajawahi kucheza mchezo wowote wa mashindano ikiwamo Ligi Kuu Bara wala mechi za kimataifa kutokana na majeraha ya muda mrefu, japo kwa sasa yupo fiti akiendelea kujifua na wenzake.

Staa huyo aliyesajiliwa Simba msimu huu kutoka ASEC Mimosas iliyowaachia pia Pacome Zouzoua na Yao Kouassi waliopo Yanga kwa sasa, ameshuhudiwa na Mwanaspoti Kwa Mkapa akiwashuhudia wenzake akiwa na rafiki zake.

Nyota huyo huenda akamaliza msimu mzima akiendelea kuwatazama wenzake akiwa jukwaani kutokana na kuchomolewa kwenye usajili wa ndani na hivyo kumzuia pia kuitumikia Simba kimataifa licha ya kuendelea kuhudumiwa na klabu kulingana na mkataba wa miaka miwili alionao Simba.

Kukosekana kwake kikosini kumefanya nafasi aliyotumika kuzibwa na mastaa wengine akiwamo Kibu Denis, Willy Onana, Saido Ntibazonkiza, Luis Miquissone, Edwin Balua, Ladack Chasambi na Saleh Kalabaka ambao wote wapo fiti na wanauwasha kweli kweli.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: