Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Konkoni: Huyo Micky Jr ni muongo sana

Konkoni 177185 Konkoni: Huyo Micky Jr ni muongo sana

Wed, 7 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Yanga SC, ambae ametolea kwa mkopo, amesema kumekuwa na Habari ambazo sio nzuri kwake na Klabu yake ya kuwa alikuwa anahudumiwa vibaya ndani ya Yanga taarifa ambazo zimesambaa kwa kasi nchini kwao Ghana, amesema sio kweli na zina nia mbaya kwake.

"Natoa shukrani kwa Yanga kwa kunipa nafasi, Yanga ni sehemu ya maisha yangu, na mara zote nilikuwa napokea mshahara wangu kwa wakati na kama ulivyo hizo taarifa sio za kweli.

"Kuhusu hizi habari sifahamu zimetokea wapi watu wanapaswa kujua kuwa nina uhusiano mzuri sana na timu ya Yanga SC, kuanzia Rais wa Klabu, Eng. Hersi hadi mtu wa mwisho kwenye timu, taarifa hizi zimesababisha mvutano kwa familia yangu.

"Nimefurahia maisha hapa na timu yangu ilikuwa inanihudumia vizuri sana, bado niko Tanzania najiandaa kujiunga na timu yangu mpya," amesema Hafiz Konkoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: