Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha wa Simba kuibukia Gor Mahia

Patrick Aussems Uchebe Kocha wa zamani wa timu ya Simba SC na AFC Leopards Patrick Aussems ‘Uchebe’

Sat, 25 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa zamani wa timu ya Simba SC na AFC Leopards Patrick Aussems ‘Uchebe’ amekiri kuwepo kwa mazungumzo na timu ya Gor Mahia kwa ajili ya kuchukua mikoba ya kocha Johnathan Mckinstry ambaye aliteuliwa kuwa mkufunzi wa timu ya taifa ya Gambia.

Kuondoka kwa McKinstry kumeibua msako wa mrithi wake huku Aussems akitajwa kuwa miongoni mwa watu wanaotarajiwa kugombea nafasi hiyo.

Aussems, ambaye kwa sasa hana klabu baada ya kandarasi yake na mahasimu wa Gor Mahia kumalizika Juni mwaka jana, ametajwa kuwa mtu anayetarajiwa kuvaa viatu vya McKinstry.

Licha ya mtaalamu huyo wa Ubelgiji kusema kumekuwa na mawasiliano, lakini hakuna ofa rasmi iliyotolewa.

Johnathan McKinstry, kocha aliyeondoka Gor Mahia, alichukua usukani Julai 29, 2022 kuiongoza Gor Mahia kutwaa taji lao la 20 la Ligi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: