Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha wa Morocco aongeza mbinu Simba

Kocha Tr Chlouha Zakaria

Fri, 28 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa makipa wa Simba, raia wa Morocco, Chlouha Zakaria ametumia muda mwingi kuucheza mchezo dhidi ya Wydad leo kwa kuwapa mbinu za ziada makipa na wachezaji wa ndani.

Kocha huyo anaijua vizuri Wydad akiwa amewahi kufanya nao kazi kaunzia mwaka 2009-2011 akiwaachia ubingwa wa ligi kuu nchini humo.

Kocha Robertinho ameliambia Mwanaspoti kuwa endapo wachezaji wake watatekeleza yote ambayo watayafanya katika maandalizi yao ya mwisho Simba itacheza nusu fainali na hilo hana wasiwasi nalo.

Robertinho alisema tayari wana kila taarifa kutoka kwa wapinzani wao akijivunia uwepo wa Zakaria na msaidizi wake wa pili Ouanane Sellami raia wa Tunisia ambaye ana marafiki wengi nchini Morocco.

"Tunajua kila taarifa za kiufundi kutoka kwa wapinzani wetu, nakiri kwamba haitakuwa mechi rahisi lakini Simba ni timu inayoweza kukabiliana na mechi ngumu, tuna wachezaji waliokomaa,"alisema Robertinho.

"Hii ni mechi kubwa kwetu na kwao lakini faida kubwa ya Simba ina makocha waliofanya kazi mataifa mengi angalia tuna Zakaria anatoka hapa alifanya kazi hapa lakini pia tuna Sellami alifanya kazi sehemu nyingi na kikubwa ana marafiki wengi hapa.

"Kitu ambacho tunawaambia wachezaji ni kuzingatia kucheza kwa nidhamu kubwa hasa wakati hatuna mpira na wakati tuna mpira, tunatakiwa kumiliki mpira na kupeleka hatari langoni kwao, tunatakiwa kufunga hapa pia hilo linawezekana kama tukiongeza umakini,"aliongeza kocha huyo Mbrazili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: