Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Yanga ataka Salim adake Dabi ya Kariakoo

Ally Salim Hg Ally Salim

Fri, 14 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa zamani Mecco na Coastal Union, na aliyekuwa kocha wa timu ya vijana ya Yanga Charles Makwaza amesema dakika 90 alizomwangalia kipa wa Simba, Ally Salim amegundua ana uwezo mkubwa na kama benchi la ufundi litamuamini hata Kariakoo Derby ya Jumapili anaweza kufanya vizuri.

“Ishu ni kumuamini kwa sababu ile mechi ndio ilionesha uwezo wake, binafsi simdai kitu na kama makocha wake wakiamua mbona anaweza kucheza hata dhidi ya Yanga?” Alihoji kocha huyo ambaye pia ni mchambuzi wa kabumbu.

“Lazima tuangalie mbali badala ya kukomaa na mtu mmoja lazima wapewe nafasi vijana kama hawa ambao kesho watasaidia kwenye mahitaji ya timu ya Taifa,” amesema Makwaza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: