Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Tanzania Prisons aanika ubovu wa Simba

Ngoma 8SR Kocha Tanzania Prisons aanika ubovu wa Simba

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Timu ya Soka ya Tanzania Prisons, Hamad Hamisi Ally amefunguka mbinu aliyoitumia kuwafunga wapinzani wao Simba SC kwenye mchezo wa juzi, Machi 6, 2024 kwenye Dimba la Jamhuri Morogoro.

Hamad amesema kuwa Simba ni wazuri kwenye kushambulia lakini wabovu kwenye kujilinda wakati wakiwa wanashambulia hivyo alitumia mpango huo kuwaadhibu bao 2-1.

“Kucheza na timu kama Simba ambayo ina wachezaji wazuri wenye uzoefu na maarifa mengi, na wanaweza kukujeruhi wakati wowote lakini ukawazuia na kuweza kupata matokeo wakiwa kwao sio jambo dogo.

“Simba kwenye kumiliki wapo vizuri asilimia 100, tuliwaacha wacheze mpira na sisi tu-attack kwa transition. Tumewapa hiyo nafasi ya kumiliki mpira na sisi tukatumia counter attack.

“Tunajua wakiwa wanashambulia, transition ya kuzuia kwao si nzuri, hicho ndicho kitu ambacho tumekisoma kwao na tukaweza kukitumia. Safu ya ushambuliaji ya Simba sio butu kwa sababu wametoka kumfunga Jwaneng Galaxy bao 6-0.

“Unapocheza na timu kubwa kama Simba, ukipata bao kipindi cha kwanza tegemea kipindi cha pili watakuja kucheza kwenye nusu yako kutafuta bao. Kwa hiyo niliwaambia vijana turudi nyuma ya mpira ili kulinda bao letu na tu-attack kwa transition,” amesema kocha huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: