Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Simba aendelea kusota rumande

Muharami Sultan Kocha Aliyekuwa Kocha wa makipa wa timu ya Simba, Muharami Sultan

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Aliyekuwa Kocha wa makipa wa timu ya Simba, Muharami Sultan (40) na wenzake watano wanaendea kusota rumande kutokana na upelelezi wa kesi inayowakabili kutokukamilika.

Muharami na wenzake watano wanakabiliwa na mashtaka nane yakiwemo ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilo 34.89 pamoja na kutakatisha fedha.

Leo Ijumaa (Novemba 17, 2023), Wakili wa Serikali Frank Michael aliieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu, kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kwamba wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Michael alitoa maelezo hayo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Kutokana na maelezo hayo, hakimu Ruboroga ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 28, 2023 itakapotajwa na washtakiwa wapo rumande kutokana na kesi hiyo kutokuwa na dhamana.

Hata hivyo, kesi hiyo ilisikilizwa kwa njia ya video huku washtakiwa wakiwa rumande.

Mbali na Muharami, washtakiwa wengine ni mmiliki wa kituo cha Cambiasso Sport Academy kilichopo Tuangoma, Kambi Zubery Seif, Said Matwiko (Magole), Maulid Mzungu 'Mbonde' (Kisemvule) ambaye ana undugu na Muharami, John John 'Chipanda' (Kitunda) ambaye kazi yake ilikuwa ni kutafuta vijana wenye vipaji na kuwapeleka Cambiasso Sport Academy pamoja na Sarah Joseph.

Awali washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na mashitaka matano, lakini Septemba 23, 2023 Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) aliwabadilishia hati ya mashtaka kwa kuwaongezea mashitaka matatu likiwemo la kutakatisha fedha na kisha kuwasomea upya mashtaka yao.

Katika shtaka la kwanza, ni kuongoza genge la uhalifu, shitaka linalowakabili watu wote ambapo inadaiwa tarehe tofauti kati ya mwaka 2016 na Novemba 4, 2022 maeneo tofauti na ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani washtakiwa hao waliongoza genge la uhalifu kwa lengo la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride.

Shtaka la pili, inadaiwa kuwa Oktoba 27, 2022 katika eneo la Kivule Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam washtakiwa hao kwa pamoja walikutwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa kilo 27.10.

Shitaka la tatu inadaiwa kuwa Novemba 4, 2023 washitakiwa, Zuberi, Zungu na Mtwiko katika eneo la Kamegele wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, walikutwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa Kilo 7.79.

Katika shitaka la nne, tano, sita na saba ambayo ni ya utakatishaji fedha yanayomkabili Kambi inadaiwa kuwa Aprili 15, 2021 katika wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam alinunua magari manne aina ya TATA yenye jina la Safia Group of Companies LTD huku akijua mali hizo zilipatikana kwa kosa la kuongoza genge la uhalifu.

Katika shitaka la nne inadaiwa kuwa Aprili 20,2021 Kambi alinunua gari aina ya TATA yenye jina Safia Group of Companies LTD akijua mali hiyo ilipatikana kwa kosa la kuongoza genge la uhalifu.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: