Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Jwaneng aidharau Simba, awahofia Asec

Morena Ramoreboli Jwaneng.jpeg Morena Ramoreboli, Kocha mkuu wa klab ya Jwaneng Galaxy

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Simba SC na Wydad Club wakikutana wikiendi hii kufufua matumaini ya kusonga mbele katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha wa Jwaneng Galaxy ambayo inashika nafasi ya pili kundi B nyuma ya ASEC ameonekana kuihofia ASEC kuliko klabu nyingine yoyote katika kundi hilo.

Akizungumza kuelekea mchezo wa Jumamosi dhidi ya Asec Morena Ramoreboli anasema;

"Mwanzoni katika hatua ya upangwaji wa makundi, baada ya kuliona kundi letu tulidhani upinzani mkubwa utakuwa kwa Timu zilizokuwa Africa Super League (Wydad Ac & Simba Sc) lakini kwa mazingira yalivyo sasa ni wazi hawa wote wawili hata wasipofuzu kucheza Robo Fainali hawatojilaumi kama ilivyo kwetu (Jwaneng Gallaxy & Asec Mimosas)"

"Kwasasa (Jwaneng Galaxy & Asec Mimosas) ndio tuna nafasi nzuri zaidi ya kufuzu kucheza Robo Fainali katika kundi hili msimu huu na nikiri Asec Mimosas ndio Timu pekee inayotunyima usingizi kupata Alama mbele yao"

"Tutapambana tofauti na michezo iliyopita dhidi ya Wydad na ule wa Simba kwani tunafahamu ili kujihakikishia kwamba tupo salama kucheza Robo Fainali ni lazimatusikubali Asec ashinde hapa Botswana."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: