Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiungo Punda na laana ya wabeba mizigo

Mzamiru Raja Simba Kiungo Punda na laana ya wabeba mizigo

Fri, 4 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni kama vile wabeba mizigo wasivyothaminiwa pale Ubungo, atakuambia leta mzigo wako pasipo kujali wa kilo ngapi utampa na kumuona akiubeba peke yake, utahisi mzigo ni rahisi

Ataufikisha salama kabisa mzigo wako na kumlipa pesa ndogo pesa ambayo haitoshi hata kununua mkate wa asubuhi ili akifariji kinywa chake.

Hapa ninawazungumzia wabeba mizigo hawa watakuaminisha kuwa kazi ya kubeba mizigo ni kazi rahisi na ukaamini. Kwanini usiamini wakati jasho lao halionekani hadharani, akimaliza kubeba mzigo wako ataondoka zake wala hataki kusifiwa.

Yupo binadamu mmoja pale Leicester City anaitwa Wilfred Ndidi alifanya kazi zote chafu pale kati, Bahati mbaya hakuimbwa sana ni kama vile wabeba mizigo wa ubungo wasivyosifiwa baada ya kazi mzito.

Sina kumbukumbu mara ya mwisho kwa kiungo namba sita kuchukua Ballon d’or labda unaweza kunikumbusha, kila siku sifa zitaenda kwa Hallaand kwa magoli yake maridadi na kulisahau jasho la Rodri

Ngolo Kante licha ya kusifiwa kwa kiwango chake bora hajawahi kunusa hata tatu bora kwenye orodha ya wachezaji bora wa Ballon d'or , Kante atakosa Ballon d’or sio kwa sababu hajafanya vizuri, hapana ni laana ya wabeba mizigo bado inamfuata

Hapa Tanzania tuna mtu anaitwa Mzamiru wanamuita Kiungo Punda, unaijua kazi ya punda ni kubeba mizigo ambayo mwanadamu hawezi kubeba hasa katika mazingira magumu, basi Kiungo Punda ramani yote ya vita pale Simba lakini jasho lake linasaulika mapema, baada ya mechi sifa zote zitaenda kwa Jean Baleke kwa bao lake la tiki taka.

Nani atalikumbuka jasho la Zawadi mauya baada ya kushuhudia amapiano za Skudu juu ya mpira? Laana ya wabeba mizigo bado inawafuata sana hawa watu. Tunawasahau mno.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: