Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipa wa Wydad naye kama Manula tu!

Tagnaouti Kipa wa Wydad naye kama Manula tu!

Fri, 28 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya kuonekana akifanya mazoezi mepesi na wenzake kambini, kuna kila dalili golikipa namba moja wa Wydad AC, Ahmed Reda Tagnaouti akaendelea kukosekana kwenye mechi ya leo dhidi ya Simba baada ya kufahamika kwamba bado majeraha aliyokuwa nayo hayajapona kwa asilimia 100.

Tagnaouti mwenye urefu futi 6 na inchi 4, alifanyiwa opereseheni ya goti Machi 30, 2023 na ndiyo maana alikosekana katika mechi mbili zilizopita za Wydad ambazo zilikuwa dhidi ya JS Kabylie na Simba.

Kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula anasumbuliwa na nyonga ambapo mapaka sasa amekosa michezo miwili ya Ligi Kuu Bara (dhidi ya Ihefu na Yanga), kombe la shirikisho la ASFC mmoja dhidi ya Ihefu na mmoja wa CAF dhidi ya Wydad.

Golikipa namba mbili, Yousef El Mutie ndiye anayetarajiwa kukaa langoni wakati mabingwa hao watetezi wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika #CAFCL watakapocheza Mchezo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 4 usiku kwa saa za Afrika mashariki na kwa saa za Afrika ya Kaskazini itakuwa saa 2 usiku katika dimba la Mohammed V nchini Morocco.

Katika mchezo wa kwanza wa robo fainali uliopigwa Jumamosi iliyopita katika Dimba la Mkapa, Dar, Simba waliibuka na ushindi wa bao 1-0 na kuwapa matumaini ya kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: