Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipa Mbrazil kuvunjiwa mkataba, Dauda awataja 'scouting' wa Simba

Hatma Ya Kipa Mbrazili Wa Simba Kujulikana Leo Kipa Mbrazil kuvunjiwa mkataba, Dauda awataja 'scouting' wa Simba

Tue, 1 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba imefanya maamuzi magumu ya kumpiga chini kipa Mbrazili Jefferson Luis aliyesajiliwa hivi karibuni kwa madai ya kuwa amepata majeraha makubwa, hivyo amesitishiwa mkataba kwani atakuwa nje kwa muda mrefu.

Akizungumzia sakata hilo, mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Shaffih Dauda amesema amesema kuwa anaamini Idara ya Scouting ya SImba ilifanya kazi kulingana na mahitaji ya klabu lakini kilichotokea kwa kipa huyo kuumia ni kinyume na matarajio yao.

“Watu ambacho hawajaelewa, Simba ina idara ya scouting ambao wanafanya kazi ya kutafuta wachezaji, mimi sitaki kuamini kwamba huyu kipa alikuja katika mazingira ambayo ni ya Kiswahili Swahili.

“Labda utuambie kwamba ile Idara iliundwa tu kwa ajili ya kutengeneza PR na si kwa ajili ya kufanya kazi inayotakiwa kufanywa na idara husika ya scouting.

“Ninaamini watu wa scouting walifanya kazi ya kumpata yule kipa wakiamini ni aina ya kipa ambaye alikuwa anatakiwa kulingana na mahitaji ya klabu.

“Ishu ya majeruhi naamini imetokea kwa sababu mchezaji amejiunga na kambi na amefanya mazoezi.

“Nimeuliza baadhi ya watu waliopo Uturuki wamenithibitishia kuwa ni kweli kipa alipata majeraha yatakayomweka nje kwa muda mrefu. Simba haikuwa na namna zaidi ya kufanya mbadala kutafuta kipa mwingine,” amesema Shffih Dauda.

Hata hivyo, Ofisa Habari Simba SC, Ahmed Ally amesema ripoti ya daktari itakayotolewa juu ya kipa wao Luis aliyeumia mazoezini nchini Uturuki ndiyo itakayoamua juu mustakabali wake kwenye klabu hiyo. Amedai ikiwa majeraha yatamweka nje kwa muda mrefu, watamuacha," amesema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: