Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kila mtoto kulipa kiingilio Kwa Mkapa, usiingie na silaha uwanjani

Uwanja Wa Mkapa Ksamd Kila mtoto kulipa kiingilio Kwa Mkapa, usiingie na silaha uwanjani

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) imewataka mashabiki wanaopenda kwenda uwanjani na watoto wao kushuhudia Dabi ya Karikaoo wawakatie tiketi ili wapate nafasi ya kukaa.

Keshokutwa Jumapili, Simba itaikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, jijini Dar es Salaam ikiwa ni dabi yao ya pili msimu huu wa Ligi Kuu Bara baada ya ile ya Ngao ya Jamii iliyochezwa Agosti jijini Tanga, Simba ikibeba ngao hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Habari wa TPLB, Karim Boimanda akidai kwamba wamepokea malalamiko ya mashabiki wanaokosa nafasi ya kukaa kwenye mechi kubwa kama hizo kwani viti vyao hukaliwa na watoto ambao hawana tiketi.

Boimanda amesema ili watoto wakae kwenye viti basi ni lazima kila mzazi anayekwenda uwanjani na mtoto akate tiketi kwa ajili ya mwanaye.

"Kumekuwepo na malalamiko ya mashabiki kukosa viti uwanjani, hii ni baada ya mashabiki wanaoenda uwanjani na watoto kutumia viti ambavyo tayari vimelipiwa na mashabiki wengine, hivyo basi ili wote kufurahia soka basi atakayekwenda uwanjani na mtoto ama watoto atalazimika kuwakatia tiketi zao ili wakate kwenye viti," amesema Boimanda

Kuhusu usalama, Boimanda aliwataka mashabiki wanaokwenda na silaha uwanjani kuzisalimisha kituo cha polisi kilicho karibu na uwanja huo na baada ya mechi watafuata silaha zao.

"Kuna mashabiki wanaingia na silaha uwanjani, hivyo kwa yeyote anayemiliki silaha na anatembea nayo basi siku hiyo atalazimika kuacha kituo cha Polisi maana hataruhusiwa kuingia nayo, mashabiki watakaguliwa, maana kule ndani usalama utakuwepo wa kutosha kutoka Jeshi la Polisi."

Boimanda amesema mageti siku hiyo yatafunguliwa kuanzia saa 4:00 asubuhi hivyo amewataka mashabiki kukata tiketi mapema ili kuepuka usufumbufu na wale watakaopewa mialiko maalumu kuhakikisha hawagawi mialiko yao kwa mtu mwingine.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: