Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kila la kheri Simba kwenye historia mpya

Simba Full Squad .jpeg Kila la kheri Simba kwenye historia mpya

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Leo ndio leo kwenye historia ya soka la barani Afrika. Simba inakwenda kuandika historia mpya katika ufunguzi wa wa michuano ya African Football League ambayo yanazinduliwa kwenye |Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Klabu hiyo itakuwa uwanjani kufungua michuano ambayo inaanza kwa mara ya kwanza barani humu. Kwa hakika ni kitu cha kujivunia kwa klabu hiyo na Taifa la Tanzania kwa ujumla.

Simba inakuwa ni mojawapo kati ya klabu nyingine saba ambazo zinaenda kuandika kitu kipya kwenye michuano hiyo barani Afrika kwa kushiriki katika mchezo wa kwanza kati yake na Al Ahly ya Misri.

Mashindano hayo yanashirikisha klabu nyingine saba za barani Afrika sambamba na klabu nyingine za Petro de Luanda, TP Mazembe, Enyimba na Al Ahly, Wydad AC, Mamelody Sundown na Esperance de Tunis.

Awali michuano hii ilitakiwa kuanza katika Bara la Ulaya mwaka 2021 ikiitwa European Super League (ESL) lakini ilikutana na upanzani mkali katika uanzishwaji wake. Kumekuwa na sababu nyingi za kukwama kwake ikiwemo msukosuko kwenye Ligi Kuu, lakini masuala makubwa ni ushindani wa wasomi ambao walidai mashandano hayo yangeondoa ushindani.

Zaidi ilidaiwa kwamba wamiliki wa klabu zilizotakiwa kushiriki walionekana kuchochewa zaidi na fedha za mashindano hayo ambazo zilikuwa nyingi sana.

Pia, kulikuwa na wasiwasi kwamba ESL ingefunika ligi za kitaifa barani Ulaya. Msukosuko huo wa kupinga kutangazwa kwa mipango ya ligi hiyo ulisababisha klabu tisa kati ya zilizotakiwa kushiriki, vikiwemo klabu sita za Ligi Kuu England, kutangaza nia ya kujiondoa.

Wazo hilo lilipoletwa Afrika halikukutana na upanzani wowote na leo tunashuhudia uzinduzi wake, huku Tanzania ikiwakilishwa na Simba ambayo katika miaka ya mitano imefika robo fainali ya michuano ya Afrika mara nne. Katika ushiriki wa michauno hiyo Simba inadaiwa 2.5 bilioni kwa ajili ya maandalizi na Shirikisho la soka la Afrika (Caf).

Mchezo wa Simba dhidi ya Al Ahly ambao una hadhi ya robo fainali utakuwa ni wa mtoano, ambapo baada ya kupigwa jijini Dar es Salaam utarudiwa jijini Cairo, Misri na mshindi wa jumla atasonga mbele kwa hatua ya nusu fainali.

Katika kuipa hamasa timu hiyo ya Tanzania kuweza kufanya vizuri, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameahidi kununua kila bao la Simba kwa Sh 10 milioni.

Kitu kikubwa katika ufunguzi huu, Watanzania tunatakiwa kuonesha umahiri katika maandalizi kwa kuwa kutakuwa na vyombo vya habari kutoka katika mataifa mbalimbali.

Pia, kutakuwa na wageni wengi wa kimataifa ambao watataka kuona uwezo wa Watanzania katika kuandaa matukio makubwa kama haya. Ikumbukwe Tanzania, Uganga na Kenya zimefanikiwa kupata uenyeji wa kundaa mashindano ya Afcon 2027. Mashabiki wa Simba na klabu kwa ujumla wanatakiwa kuonesha ukubwa wao katika mashindano hayo baada ya kuaminiwa. Kila la heri Simba Sports.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: