Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kila la heri Mnyama, ASEC anawezekana

Simba Wamerejea Nchini Kila la heri Mnyama, ASEC anawezekana

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Presha kubwa inakuwa kwa mashabiki ambao mara kadhaa wanakuwa na mihemko kutokana na timu zao wao wanataka ushindi tu na si vinginevyo lakini mpira hauko hivyo.

Timu zote zinafungwa duniani kwahiyo ni kuamua tu kuwa watulivu ili wasizidi kuharibu huko mbele kwasababu bado shughuli ni nzito katika mashindano ya kimataifa hivyo sapoti ya mashabiki ndiyo kubwa inayohitajika kwa sasa na si vinginevyo japo kuumia kupo ila wanatakiwa kustahamili.

Kama kweli wewe ni shabiki wa mnyama umejifungia zako chumbani na kuumia au ukitoka nje ndiyo wa kwanza kuisema timu yako kwa mabaya au vyovyote ujue hapo hujengi unazidi kubomoa na kwa mtani yeye ndiyo burdani yake.

Usingoje uambiwe uende uwanjani nenda kasapoti timu yako mengine ya kimpira yapo tu na njia sahihi zipo za kufikisha kama ni malalmiko au maoni yoyote yale.

Na ndiyo mana afisa habari wenu anakesha mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuwarudisha muendelee kuwa wamoja viongozi wanafanya vikao siyo kwamba hawaelewii au hawatambui yanayoendelea , wanajua kila kitu kikubwa ni subra na imani kuhusu timu yenu.

Tarehe 25 si mbali kuna kibarua kizito na mashabiki mtakiwa uwanjani mkatoe sapoti ya hali na mali kuwapa nguvu wachezaji wenu ili wafanye vizuri katika mchezo huo uliopo mbele kwa sasa, siyo wakati wa kunyoosheana vidole.

Kila la kheri Mnyama katika mashindano ya kimataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: