Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiemba: Simba kwa sasa haichezi vizuri

Amri Kiemba Simba Sc Kiemba: Simba kwa sasa haichezi vizuri kama tulivyoizoea

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa zamani wa Simba SC na Yanga SC, Amri Kiemba amesema kuwa timu ya Simba kwa sasa haichezo soka la kuvutia kama ilivyokuwa imezoeleka kipindi cha nyuma.

Kiemba ambaye ni mchambuzi wa masuala ya soka nchini amesema hayo mara baada ya Simba kufuzu hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos huku akidai kuwa identity ya soka la pasi la Simba imepotea kabisa.

"Ni kweli sasa hivi Simba haichezi vizuri! Inashindwa kucheza ndani ya kiwanja kwa namna ambavyo ilikuwa imezoeleka. Simba ina utamaduni wake wa namna ya kucheza.

"Sasa hivi imepoteza utambulisho wake wa uchezaji ‘identity’ kwamba ikiwa haina mpira inachezaje na ikiwa na mpira inachezaji.

"Ukiangalia Simba ina wachezaji wazuri uwanjani lakini wanafanya nini kama timu tatizo ndio linaanzia hapo. Na hicho ndio kina leta tofauti ya Simba na Yanga kwa sasa.

"Kwa hiyo mashabiki kusema timu yao haichezi vizuri hawapo mbali na ukweli lakini kwenye mafanikio bado timu imeendelea kufanya kilekile ambacho imekuwa inakifanya.

"Hoja ya kwamba Simba imekutana na mpinzani mgumu sio ya msingi sana kwa sababu tayari Simba imeshacheza na wapinzani wagumu zaidi ya Power Dynamos," amesema Amri Kiemba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: