Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kapombe aacha msala Uhamiaji

Shomari Kapombe Msala.jpeg Shomari Kapombe

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kuchakazwa mabao 3-1 na Simba, Kocha wa Uhamiaji FC, Abdi Saleh amesema beki wa Wekundu hao, Shomari Kapombe alikuwa mwiba huku akikubali shoo yake.

Uhamiaji ikicheza juzi mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa New Amaan, visiwani hapa ilikubali kipigo hicho huku Kapombe akionyesha kiwango bora na kocha huyo alisema alikuwa akipambana na kuitendea haki nafasi yake muda wote wa mchezo.

Alisema kutokana na uimara wa beki huyo wa kulia, aliwanyima nafasi nyota wake kupenyeza mipira ili kulifikia lango la Wekundu na kujikuta wakilala kichapo hicho.

“Kapombe alikuwa bora muda mwingine alipanda na kushuka kudhibiti mashambulizi, hakutoa nafasi kwa straika wetu kupenyeza mipira, kwangu ndiye amekuwa mwiba kwetu,” alisema kocha huyo.

Kuhusu kikosi chake, kocha huyo alisema licha ya vijana wake kutokuwa katika muunganiko kutokana na mapumziko waliyokuwamo, lakini walionyesha ubora na inampa matumaini ya kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu.

Alisema kwa sasa wanaendelea na programu ndogo ndogo wakisahihisha makosa hasa eneo la beki, wakisubiri kurejea kwa mashindano ili kufanya vizuri.

“Tulikuwa mapumziko ndio maana hatukuonyesha makeke sana, lakini tunaona uelekeo mzuri wa kufanya vizuri na mechi hii imetupa kujiamini na kubaini makosa yetu,” alisema kocha huyo.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: