Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanoute kaanza na rekodi yake kwa Benchikha

Sadio Kanoute Second Goal.jpeg Kanoute kaanza na rekodi yake kwa Benchikha

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa kazi ngumu, Sadio Kanoute ameanza na rekodi yake mbele ya kocha mpya, Abdelhak Benchikha kwa kuwa nyota wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano katika mchezo wa kwanza kukaa benchi.

Ikumbukwe kwamba Benchikha ni mrithi wa mikoba ya Roberto Oliveira, mchezo wake wa kwanza kukiongoza kikosi cha Simba ilikuwa Desemba 2, alishuhudi ubao ukisoma Jwaneng Galaxy 0-0 Simba.

Kwenye mchezo huo ni Kanoute alikuwa wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano dakika ya 45 alipotembeza buti la kimyakimya kwa mchezaji wa Jwaneng Galaxy. Inakuwa ni kadi ya pili kwa Kanoute ya kwanza alionyeshwa mchezo dhidi ya ASEC Mimosas.

Nyota mwingine wa Simba aliyeonyeshwa kadi ya njano kwenye mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy ni beki wa kazi ngumu Henock Inonga ilikuwa dakika ya 46 muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza.

Wakati hayo yakitokea, kipa Ayoub Lakred ni mchezo wake wa kwanza katika hatua ya Ligi ya Mabingwa Afrika kukomba dakika 90 bila kufungwa kwa kuwa kwenye mechi tatu alizocheza zote alitunguliwa.

Ilikuwa Power Dynamos 2-2 Simba, Simba 1-1 Power Dynamos na Simba 1-1 ASEC Mimosas kakutana na clean sheet mchezo wa nne, Jwaneng Galaxy 0-0 Simba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: