Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kakolanya: Si kwenda Simba kushindania namba

Beno Kakolanya Bb Beno Kakolanya

Sat, 8 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa kipa namba mbili Simba SC, Beno Kakolanya amezungumza na kusema msimu uliopita ulikuwa mzuri japo matarajio ya Simba hayakutimia kutokana na kudondosha pointi na wapinzani walikuwa wakishinda

Kakolanya amekuwa akihusishwa kwenda kumwaga wino Singida Fauntain FC alikovuta mkwanja mrefu, ingawa akiulizwa hilo anaishia kucheka na wala halizungumzii kabisa.

Amefunguka na kuisifia Yanga ya msimu uliopita kwa mafanikio waliyoyapata ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu, ASFC, Ngao ya Jamii na kufika fainali Kombe la Shirikisho Afrika na kuwa mshindi wa pili

"Yanga walikuwa vizuri haiwezi kupingika na walistahili kupata ubingwa, msimu ujao simba watajipanga zaidi ili kurudisha heshima ya makombe," amesema Kakolanya na kuongeza.

"Nilienda Simba kusaidia timu na kusaidiana na Manula pamoja Ally, sikwenda kushindana namba na Manula na mimi nilikuwa kipa namba mbili na Ally ulikuwa ni muda wake wakucheza na huwezi kupingana na mwalimu

Kakolanya amesema anaona msimu ujao utakuwa mgumu kwasababu timu zinapambana kusajili na hana mashaka na uwezo wangu nitafanya vizuri msimu ujao kimataifa

"Najiamini timu yoyote nitakayoenda kwenye mashindano ya Kimataifa sina mashaka na uwezo wangu na watu wananijua lakini msimu uliopita nimecheza mechi chache kwahiyo nikisema ushindani upo nitakuwa na danganya"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: