Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaduguda: Kina Fredy, Jobe, Babacarr wapo Tandika kama utitiri

Babacarr Jobe Fredy Jobe, Babacarr na Fredy.

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba, Mwina Mohamed Seif Kaduguda 'Simba wa Yuda' amesema kuwa, viongozi wa klabu hiyo wamefanya makosa makubwa kuwasajili washambuliaji Fredy Michale, Pa Omar Jobe na kiungo Babacarr Sarr kwani hawana uwezo wa kuichezea timu hiyo.

Kaduguda ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba na Kaimu Mwenyekiti wa klabu hiyo kwa nyakati tofauti, amesema kuwa wachezaji wa kariba hiyo wanapatikana kwa wingi maeneo ya Tandika na Mwananyamala, hivyo kwa wachezaji hao ni vigumu kwa Simba kwenda nusu fainali au kuchukua ubingwa wa CAFCL.

“Viongozi wa Simba wamefeli maeneo mengi lakini nitataja moja tu la usajili, huwezi kumtoa Baleke ukamleta Fredy, ukamtoa Phiri ukamleta Jobe. Wanasimba waone wasiwe waoga kusema, hapa uongozi umeteleza lazima tukubali.

“Kama unataka kwenda nusu fainali au kuchukua ubingwa wa frika, kweli mshambuliaji ni Fredy? Eeh jamani! Kiungo Babacarr? Hawa wachezaji hawa ukienda Tandika, Mwananyamala wapo wengi tu kama utitiri au kama mvua ya mawe.

“Tuletee mchezaji Simba au Yanga ambaye unamuona huyu kwa kweli tunastahili kumlipa, lakini mchezaji ambaye Tandika yupo, Mwananyamala yupo! Halafu ukisema inakuwa nongwa? Aah jamani!,” amesema Mwina Kaduguda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: