Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaburu: Wapeni muda, mtafurahi

Kaburu Pic Data Kaburu: Wapeni muda, mtafurahi

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' amesema maingizo mapya ndani ya kikosi cha Simba yanahitaji muda zaidi ili kupata kikosi bora na cha ushindani huku akikiri kuwa usajili uliofanywa ni bora.

Simba ipo nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya kukusanya pointi tisa kwenye mechi tatu huku ikifunga mabao tisa na kuruhusu mabao mawili.

Kaburu anasema anashangazwa na baadhi ya mashabiki wa timu hiyo kushindwa kukubaliana na aina ya uchezaji wa timu yao ambayo imekuwa ikiwapa matokeo.

"Kila shabiki wa Simba matarajio yake ni kuona timu ya misimu minne nyuma ambayo imefanya mambo makubwa ligi ya ndani na kimataifa hilo linawezekana kutokana na kikoswi lakini muda unahitajika zaidi;

"Simba ina wqachezaji wazuri ukiangalia mmoja mmoja huyo Clatous Chama na Luis Miquissone waliokuwa bora misimu minne hawakuanza moja kwa moja iliwachukua muda hivyo hata sasa hawa waliopo wapewa muda watakuwa bora zaidi." anasema.

Kaburu anasema anaridhishwa na uwezo wa kikosi cha Simba huku akiweka wazi kuwa ni nadra kwa timu iliyovunjika na kusajiliwa upya kuanza na matokeo mazuri kama wanayoyapata Simba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: