Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMC, Mtibwa yazoa Wachezaji Simba SC

Simba SC BB.jpeg KMC, Mtibwa yazoa Wachezaji Simba SC

Mon, 15 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji watatu kati ya sita waliotemwa na Simba SC katika dirisha dogo, Nassor Kapama, Jimmyson Mwanuke na Shaaban ldd Chilunda wamepata dili baada ya kunaswa na Mtibwa Sugar na KMC.

Mwanuke na Kapama wametua zao Mtibwa, wakati Chilunda aliyewahi kuwika na Azam FC akisajiliwa KMC FC ili kuendeleza moto alioshindwa kuuwasha Msimbazi.

Akizungumza jijini Dar es salaam Kapama amesema ni kweli amemalizana na Mtibwa kwa mkataba wa miezi sita baada ya kuvunjiwa mkataba na Simba SC sasa atakuwa huko kuipambania timu hiyo isishuke daraja.

“Nimemalizana na Mtibwa nitacheza huko kwa miezi sita naamini ni chaguo sahihi baada ya ofa nyingi nilizokuwa nazo naamini nitapambana kwa kushirikiana na wenzangu ili kuiondoa timu hiyo kwenye hatari ya kushuka daraja.” amesema Kapama.

Wakati huohuo rafiki wa karibu wa Mwanuke amesema kuwa beki huyo amejiunga na Mtibwa kwa mkopo akitokea Simba SC.

“Mwanuke ametolewa kwa mkopo na Simba ili aweze kuisaidia Mtibwa kukwepa janga la kushuka daraja kutokana na kuwa katika nafasi mbaya,” kimeeleza chanzo chanzo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: