Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#KLABUBINGWA: Hiki hapa kikosi cha Simba vs Wydad, Chama ndani

Simba SC BB.jpeg #KLABUBINGWA: Hiki hapa kikosi cha Simba vs Wydad, Chama ndani

Tue, 19 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba ina kibarua kizito jioni ya leo Jumanne Desemba 19, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kusaka ushindi wake wa kwanza kwenye kundi B katika Ligi ya Mabingwa Afrika itakapoivaa Wydad ya Morocco.

Hadi sasa Simba ipo nafasi ya nne kwenye kundi hilo ikiwa na pointi 2 ikitoa sare mbili na kupoteza mchezo mmoja ugenini dhidi ya Wydad.

ASEC Mimosas ndio kinara wa kundi hilo akiwa na pointi saba, Jwaneng Galaxy (4), Wydad (3) na Simba ikiburuza mkia (2) ambapo kama atashinda mchezo wa leo atafikisha pointi tano.

Simba baada ya mchezo wa leo itakua imebakiza mchezo mmoja Kwa Mkapa dhidi ya Jwaneng na ugenini dhidi ya ASEC.

Hiki hapa kikosi cha Simba kinachoanza mchezo wa leo;

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: