Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

John Bocco: Tunacheza nyumbani tuna uhakika wa matokeo

John Bocco AFL Nahodha wa Simba, John Bocco

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni mchezo mkubwa kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla, utakuwa mchezo mzuri sana. Ni nafasi nzuri kwa klabu yetu na sisi wachezaji kuonesha kiwango kizuri katika mchezo huo na mashindano haya makubwa.

Tunatarajia kuonesha mchezo mzuri na wa kiungwana kwa wapinzani wetu ingawa tunajua utakuwa mchezo mgumu kwa sababu tunakutana na timu kubwa yenye wachezaji wazoefu kwenye mashindano kama haya.

Tuna imani tuna timu nzuri na wachezaji wenye uzoefu wa mechi kama hizi, tunatarajia matokeo mazuri kwa sababu tunacheza nyumbani halafu ni mchezo wa kwanza kwenye mashindano ya mtoano.

Ni kitu kikubwa na cha kujivunia kama nchi kupata nafasi ya kuandaa mechi ya ufunguzi wa mashindano haya makubwa, wachezaji tuna jukumu kubwa la kupata matokeo mazuri uwanjani kwa sababu ni mchezo wa kwanza na tunacheza nyumbani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: